Salad ya matunda

Maandalizi; dakika 20
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Kwa salad ya matunda

Chungwa moja kubwa, (nusu kwa dressing nusu kwa fruit salad)
¾ kikombe cha vipande vya strawberries
¾ kikombe cha vipande vya nanasi
¾ kikombe cha vipande vya ndizi mbivu
1 kiwi
¾ Kikombe cha embe

Kwa dressing ya maji ya machumngwa, limao na ndimu

½ chungwa
½ limao la wastani
½ ndimu
1 kijiko cha chai asali
¼ kijiko cha chai tangawizi iliyotwangwa
1½ kijiko cha chai maganda ya limao, chungwa na ndimu
¼ kijiko cha chai mbegu za maua (poppy seeds, ukipenda)

Maelekezo

Osha na kukausha limao, ndimu na chungwa. Kwa kutumia kikwangulia, kwangua maganda yake. Tengeneza 1½ kijiko cha chai cha maganda. Twanga au kwangua na tangawizi, weka pembeni

Kata kila tunda (limao, ndimu na chungwa) nusu. Kamua maji yake kwenye kibakuli, unahitaji vijiko vinne vya chakula

Ongeza asali, tangawizi na mbegu za maua (poppy seeds) kwenye machanganyiko wa juisi, changanya vizuri. Weka pembeni, au hifadhi kwenye jokofu endapo salad italiwa badae

Katakata strawberries, ndizi na kiwi vipande vya mduara. Katakata nanasi na embe vipande vidogo vidogo kiasi. Menya na katakata nusu ya chungwa

Kwenye bakuli kubwa, weka mchanganyiko wa matunda yote vizuri

Mwagia dressing (mchanganyiko wa machungwa, ndimu, limao, asali na mbegu za maua) kwenye salad. (unatakiwa kuchanganya na dressing dakika 30 kabla ya kuliwa)

Tenga kama utakavyopenda

Enjoy

5 Replies to “Salad ya matunda”

Leave a Reply