Sosi ya chocolate

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 5
Muda jumla; dakika 10

Mahitaji

Kikombe 1 cha kokoa isiyokuwa na sukari
Kikombe 1 cha sukari
Kikombe 1 cha maji ya baridi
½ kijiko cha chai chumvi
Kijiko 1 cha chakula vanilla

Maelekezo

Kwenye sufuria ya wastani, weka kakao, sukari, maji na chumvi

Karoga vizuri mpaka ichanganyike vizuri

Katika moto wa wastani, chemsha mchanganyiko kwa dakika 3 hadi 4 mpaka uwe mzito kiasi. Uzito utakuwa mwepesi kiasi, utaongezeka ikipoa.

Ipua kwenye moto, ongeza vanilla. Acha ipoe

Hifadhi kwenye jokofu katika chombo kinachofunga vizuri. Inaweza kukaa kwenye jokofu kwa muda wa mwezi mmoja

Inafaa kutumiwa kwenye maziwa, kahawa, smoothies, milkshakes, desserts, keki na vitu vinginevyo

Enjoy!

 

3 Replies to “Sosi ya chocolate”

Leave a Reply