Mkate wa nyama ya kusaga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; lisaa 1
Muda jumla; lisaa 1 dakika 10
Idadi ya walaji; 4

Mahitaji

Kwa mkate wa nyama

Nyama ya kusaga 500g/ nusu kilo
Slesi 1 ya mkate
Yai 1
Kitunguu maji 1 kidogo
Punje 3 za kitunguu saumu
Vijiko 2-3 vya chakula tomato sauce
½ kikombe maziwa
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Unaweza pia kuongeza viungo vingine utakavyopenda kama pilipili, tangawizi nk

Kwa sauce

Vijiko 3 vya chakula siki (apple cider vinegar)
Kijiko 1 cha chakula, sukari ya brown
¼ kikombe na vijiko 2 vya chakula tomato sauce

Maelekezo

Washa oven joto la 175 degrees C. Katakata kitunguu na mkate vipande vidogodogo sana. Twanga kitunguu saumu

Kwenye kibakuli kidogo, changanya sauce kwa kuweka siki, sukari na ½ kikombe tomato sauce

Changanya vizuri, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, changanya viungo vyote vya nyama

Changanya vizuri. Weka mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea, tengeneza umbo zuri la mkate

Mwagia sauce kwa juu na pande zote za mkate

Oka kwa muda wa lisaa 1, au mpaka uive

Pakua kama utakavyopenda

Ukipenda, mwagia sosi iliyobakia kwenye chombo cha kuokea kwa juu

Enjoy

15 Replies to “Mkate wa nyama ya kusaga”

    1. Maziwa ni fresh. Mboga nimechemsha tu na maji dakika 3, nikazimwagia sosi iliyobakia kwenye chocmbo cha kuokea nyama ilipoiva

Leave a Reply