Frozen Yogurt ya embe

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kugandisha; masaa 4
Muda jumla; masaa 4 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 4 embe
½ kikombe mtindi mzito, jinsi ya kutengeneza bonyeza hapa
Vijiko 2 vya chai vanilla extract
Vijiko 3 vya chakula asali

Maelekezo

Osha na kukatakata embe

Weka embe kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula kwenye freezer. Funga na kuhifadhi kwenye freezer kwa masaa 4 hadi miezi 10

Ukiwa tayari kutumia, weka embe lililoganda, mtindi, asali na vanilla kwenye food processor au blender (hakikisha blender yako ina nguvu)

Saga mpaka ilainike, kama dakika 5

Tenga iliwe mara baada ya kutengeneza au weka kwenye chombo cha kuokea mkate freezer kwa masaa mawili ukipenda iwe nzito kama ice cream.  Inaweza kukaa hadi mwezi mmoja kwenye freezer katika kontena la plastic lenye mfuniko. Kumbuka ukiweka kwenye freezer kwa muda mrefu itakuwa ngumu kiasi kulinganisha na masaa machache baada ya kutengeneza

Enjoy

Leave a Reply