Kuku wa kukaanga wenye buttermilk

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; masaa 4
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; masaa 4 dakika 35

Mahitaji

Kwa marinade ya kuku

Kilo 1 kuku
Kikombe 1 buttermilk (au kikombe 1 mtindi, vijiko 3 maji)
Vijiko 1½ vya chai kitunguu saumu
Vijiko 1½ vya chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai pilipili manga
Kijiko 1 cha chai udaha (cayenne pepper)
Chumvi kwa kuonja

Kwa unga wa kupaka

Vijiko 4 vya chakula unga wa ngano
Kijiki 1 cha chakula chicken boulloin powder au royco
Kijiko 1 cha chai curry powder
Mafuta ya kutosha kukaangia
Viungo vingine ukipenda

Maelekezo

Katakata, osha na kukausha kuku

Kwa kutumia kisu kikali, chanja kuku

Paka kuku chumvi na pilipili manga

Kwenye bakuli kubwa, changanya buttermilk, kitunguu saumu, tangawizi na udaha

Weka kuku, mchanganye vizuri na viungo

Funika na kuhifadhi kwenye jokofu kwa masaa manne, au usiku mzima

Changanya unga wa ngano, curry powder na chicken boulloin powder/ royco kwenye sahani kubwa au chombo kipana

Toa kuku kwenye buttermilk, chovya kwenye mchanganyiko wa unga, hakikisha unga umeshika vizuri

Kwenye kikaango katika moto wa wastani, chemsha mafuta. Yakichemka ongeza kuku aliyepakwa mchanganyiko wa unga. Pika kwa dakika 5 hadi 7 upande mmoja

Geuza upande wa pili, kaanda kwa dakika nyingine kama 5, au mpaka aive vizuri

Toa kwenye mafuta, weka kwenye sahani yenye tissue ili mafuta yachuje. Unaweza pia kuweka kwenye chujio la bati ili mafuta yachuje

Pakua kama utakavyopenda

4 Replies to “Kuku wa kukaanga wenye buttermilk”

    1. Cayenne pepper, ile kama pilipili imesagwa unakuwa kama unga mwekundu. Kama hauna usijali, unaweza tumia paprika au usitumie kabisa

Leave a Reply