Frozen yogurt ya strawberries na ndizi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kugandisha; masaa 6
Muda jumla; masaa 6 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 3 vya strawberries
Ndizi mbivu 2 za wastani
½ kikombe mtindi mzito, jinsi ya kutengeneza bonyeza hapa
Kijiko 1 cha chai vanilla extract

Maelekezo

Osha na kukatakata matunda

Weka matunda kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula kwenye freezer. Funga na kuhifadhi kwenye freezer kwa masaa 4 hadi miezi 12

Ukiwa tayari kutumia, saga viungo vyote kwenye food processor au blender (hakikisha blender yako ina nguvu). Saga mpaka ilainike, kama dakika 5

Mwagia mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea mkate au kontena, sawazisha ulingane vizuri kwa juu

Weka kwenye freezer kwa masaa 2, au mpaka igande ila isiwe ngumu ukichota. (Kama utahifadhi kwa muda mrefu, funika na mfuniko au nailoni ya kufunikia chakula. Ukitaka kula acha iyeyuke kiasi kwa dakika kama 5 kabla hujachota)

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

2 Replies to “Frozen yogurt ya strawberries na ndizi”

    1. Mtindi unaweka wakati unasaga kwenye blender. Kwenye blender itakuwa ni matunda yaliyoganda, mtindi na viungo vingine vinavyohitajika

Leave a Reply