Kachumbari ya strawberries

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Kikombe 1 strawberries
½ kikombe nyanya
Pilipili kichaa nyekundu 1
Vitunguu vya majani 3
¼ kikombe majani ya giligilani
Maji ya ndimu 1
½ kijiko cha chai tangawizi
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Katakata strawberries, nyanya na pilipili vipande vidogovidogo vya mraba. Katakata majani ya giligilani na majani ya kitunguu. Twanga na tangawizi

Katika bakuli kubwa, changanya viungo vyote. Kamulia ndimu, ongeza na chumvi na pilipili manga kiasi utakachopenda

Tenga kama utakavyopenda. Inapendeza sana kuliwa na nyama choma, samaki wa kuoka au kuchoma au hata vyakula vingine tofauti

Enjoy

Leave a Reply