Mtindi mzito/ Greek yoghurt

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kusubiri; lisaa 1
Muda jumla; Lisaa 1 dakika 5

Mahitaji

Mtindi
Tissues za jikoni
Chujio kubwa

Maelekezo

Weka chujio juu ya sahani au bakuli kubwa. Weka tissues za jikoni kwenye chujio, zisukume kwa chini zikae kwa chini kabisa

Weka mtindi kwenye tissues za jikoni

Weka tissue nyingine kwa juu ya mtindi

Acha maji yachuje kwa muda kama wa lisaa moja. Ikikaa muda mrefu mtindi utakuwa mzito Zaidi. Endapo utaiacha Zaidi ya lisaa moja, weka ndani ya friji mpaka utakapohitaji

Toa tissue ya juu

Inua tissue zilizobeba mtindi, toa kwenye chujio, mimina mtindi kwenye bakuli nyingine

Koroga mtindi mpaka ulainike

Tumia kama inavyohitajika

10 Replies to “Mtindi mzito/ Greek yoghurt”

    1. Ndio, mtondi wowote unaweza kuchuja. Kwa smoothie au raita ni vizuri kuchuja kuondoa maji ili kuweka uzito isiwe majimaji

Leave a Reply