Ice cream ya cookies

Kutengeneza; dakika 15
Kugandisha; masaa 3-4
Muda jumla; Masaa 3-4 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 2 whipping cream
Kijiko 1 cha chakula vanilla
Kikombe 1 maziwa ya Sona, au kutengeneza nyumbani bonyeza hapa
Cookies za chocolate 20

Maelekezo

Weka cookies kwenye mfuko wa plastic wa kuhifadhia chakula. Acha hewa itoke, funga mfuko. Tumia kikaangio au kimti cha kusukumia chapati kuvunjavunja cookies, ila zisipodeke sana, ziwe na vipande vikubwa vikubwa, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, kwa kutumia mashine ya kusagia keki, piga cream na vanilla pamoja mpaka iwe nzito kabisa

Ongeza maziwa mazito/ maziwa ya sona, koroga vizuri kabisa

Weka cookies zilizovunjwavunjwa, koroga kiasi kwa kutumia kijiko siyo mashine

Mwagia mchanganyiko kwenye contena ya plastic yenye mfuniko au chombo cha kuokea mkate cha bati

Gandisha kwa masaa 3-4; au usiku kucha mpaka igande vizuri kabisa

Enjoy

11 Replies to “Ice cream ya cookies”

  1. Tumia blender, changanya cream, vanilla na maziwa mazito kwenye blender speed ya juu kwa sekunde 30 hadi dakika mo; au hadi iwe nzito na creamy. Ukitoa ndio uweke cookies ukiroge kwa kijiko siyo yana. Au tumia pia mkono, piga cream na vanilla kwa kichuma cha kukorogea keki hadi cream iwe nzito kabisa, ongeza maziwa endelea kupiga hadi ichanganyike vizuri, ndio uweke cookies mwishoni

 1. Jane ur blog ni msaada sana ubarikiwe ktk kaz za mikono yako, mm ni mgeni wa hivi vitu, whipping cream inapatikana wapi na ikoje na ukisema maziwa mazito yakoje na yanapatikanaje, kifupi msaada tafadhali kwa mgeni ka mimi!

   1. Asante kwa feedback, maziwa mazito ya kopo ulotumia ndio nlitaka kujua ni yapi..sijaelewa pia hapo! Au ndio hiyo link umenitumia jinsi ya kujifunza kuyatengeneza

    1. hapana, pole. Nimekuelewa sasa hivi, ni yale maziwa ya kopo mazito na matamu sana, kuna yanayoitwa Sona, taangalia majina mengine nikutumie. Nitaweka pia recipe ya kutengeneza mwenyewe nyumbani wiki hii

     1. Nashkuru sana, ukipata majina tupostie tujue tujifunze, manake tumeulizana wengine tunadanganyana. Ubarikiwe!

 2. Hallow Jane, asante sana kwa darasa lako linatusaidia sana, nipo najaribu hii Ice-cream na nmefika mahali pa kuweka whipping cream na vanila ili nikoroge, lakini ipo in form of powder sasa nakorogaje na vanila au natia maji?

  1. Kama ni powder utahitaji kuweka na maji. Angalia kwenye box wanataka vipimo kiasi gani, nimeangalia mtandaoni naona kikombe 1 cha maji na kikombe 1 cha powder. Jaribu kikombe na nusu maji na kikombe na nusu powder kuona kama mchanganyiko utakuwa vikombe 2

Leave a Reply