Kachumbari ya tango na mtindi

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Kikombe 1 tango
¾ kikombe mtindi
Vijiko 2 vya chakula majani ya giligilani
Vijiko 2 vya chakula majani ya nanaa
Pilipili kichaa 1 (au pilipili mbuzi ukipenda ya kuwasha)
Kijiko 1 cha chakula maji ya limao
Chumvi  kwa kuonja

Maelekezo

Menya na kukatakata tango; katakata pilipili, giligilani na nanaa

Saga majani ya nanaa, majani ya giligilani, maji ya limao na pilipili kutengeneza rojo

Kwenye bakuli changanya mtindi na rojo ya viungo vingine ulivyotengeneza. Ongeza tango na chumvi

Enjoy na chakula chochote hasa briyani na pilau

Leave a Reply