Smoothie ya strawberry na asali

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kusubiri; masaa 4
Muda jumla; masaa 4 dakika 10

Mahitaji

Vikombe 3 strawberries
Kikombe 1 mtindi mzito, kwa recipe bonyeza hapa
Kijiko 1 cha chakula asali
½ kijiko cha chai vanilla (ukipenda)
Vikombe 1½ maziwa fresh

Maelekezo

Osha matunda

Katakata matunda

Weka matunda kwenye mfuko wa kuwekea chakula kwenye jokofu. Funga na hifadhi matunda kwenye freezer kwa masaa 4. Yanaweka kukaa hadi miezi 12

Ukiwa tayari kutumia, weka maziwa fresh, mtindi, asali, vanilla na matunda yaliyoganda kwenye blender au mashine ya kusagia chakula. Saga hadi yalainike vizuri

Enjoy

 

2 Replies to “Smoothie ya strawberry na asali”

Leave a Reply