frozen yoghurt yembe na tui la nazi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kugandisha; masaa 6
Muda jumla; masaa 6 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 3 embe
½ kikombe tui la nazi
½ kikombe mtindi mzito; kwa recipe bonyeza hapa
Vijiko 2 vya chakula asali

Maelekezo

Osha na kukatakata embe

Weka embe kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula kwenye freezer. Funga na kuhifadhi kwenye freezer kwa masaa 4 hadi miezi 10

Ukiwa tayari kutumia, weka embe lililoganda, mtindi, asali na tui la nazi kwenye food processor au blender (hakikisha blender yako ina nguvu)

Saga mpaka ilainike, kama dakika 5

Weka mchanganyiko kwenye chombo cha kuokea mkate au container yenye mfuniko. Sawazisha kwa juu kuwe na uwiano

Gandisha kwa masaa 2, au mpaka ingande ila isiwe ngumu sana ukichota na kijiko. Endapo utaigandisha usiku mzima au kwa muda mrefu, funika na mfuniko katika container, au kwa chocmbo cha mkate funika na nailoni za kufunikia chakula. Ukitaka kutumia, acha iyeyuke kwa dakika kama tano ili iwe laini kuchota na kijiko

Chota na kijiko kikubwa kupakua kwenye kibakuli. Pamba na chochote utakachopenda

 

Enjoy

Leave a Reply