Salad ya kuku wa limao na viungo tofauti

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; Masaa 2 dakika 30

Mahitaji

Kwa marinade/dressing

Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni
¼ kikombe maji ya limao
Vijiko 2 vya chakula maji
Vijiko viwili siki (red wine vinegar)
Vijiko 2 vya chakula majani ya giligilani
Vijiko 2 vya chai majani makavu ya mrehani (basil)
Vijiko 2 vya chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai oregano
Kijiko 1 cha chai chumvi
Pilipili manga kwa kuonja
500g/ nusu kilo minofu ya kuku

Kwa salad

Vikombe 4 majani ya salad chaguo lako
½ tango
Nyanya 1
½ kitunguu maji
Parachichi 1
¼ kikombe matunda ya mzaituni (olives)
Majani ya vitunguu

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako

Twanga kitunguu saumu, kamua limao na katakata majani ya giligilani, weka pembeni

Kwenye bakuli ndogo, changanya vizuri viungo vyote vya marinade/ dressing

Kwenye bakuli kubwa, changanya kuku na nusu ya marinade/ dressing, hakikisha kuku kakolea viungo vizuri

Funika bakuli, acha viungo vikolee kwa dakika 15-30, au mpaka masaa 2 kwenye jokofu. Hifadhi marinade/ dressing iliyobakia kwenye friji kwa kutumia kwenye salad

Osha na kukausha majani ya salad

Katakata nyanya, matunda ya mzaituni, parachichi, tango na vitunguu vya majani

Kwenye kikaangio katika moto mkali kiasi, chemsha mafuta. Ongeza kuku kwenye mafuta

Acha aive kila upande mpaka awe na rangi ya kahawia na ameiva vizuri

Ipua kuku, acha apoe

Wakati kuku anapoa, pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda

Katakata kuku vipande vyembamba

Weka kuku kwenye bakuli. Nyunyizia marinade/ dressing iliyobakia kwa juu na majani ya kitunguu kwa juu

Enjoy

One Reply to “Salad ya kuku wa limao na viungo tofauti”

Leave a Reply