Ice cream ya cookies na ndizi

Kutengeneza; dakika 15
Kugandisha; masaa 6
Muda jumla; Masaa 6 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 2 whipping cream
Kijiko 1 cha chakula vanilla
Kikombe 1 maziwa ya Sona au tengeneza kwa recipe hapa
Cookies za chocolate 20
Ndizi mbivu 2
Vijiko 2 rangi ya njano (ukipenda)

Maelekezo

Weka cookies kwenye mfuko wa plastic wa kuhifadhia chakula. Acha hewa itoke, funga mfuko. Tumia kikaangio au kimti cha kusukumia chapati kuvunjavunja cookies, ila zisipondeke sana, ziwe na vipande vikubwa vikubwa, weka pembeni

Ponda ndizi zilainike vizuri kabisa, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, kwa kutumia mashine ya kusagia keki, piga whipping cream, rangi ya njano (endapo utatumia rangi) na vanilla pamoja mpaka iwe nzito kabisa

Ongeza maziwa ya Sona, koroga vizuri kabisa

Weka ndizi zilizopondwa, koroga vizuri

Weka cookies zilizovunjwavunjwa, koroga kiasi na kijiko

Mwagia mchanganyiko kwenye contena ya plastic yenye mfuniko au chocmbo cha kuokea mkate cha bati

Gandisha kwa masaa kadhaa au usiku kucha mpaka igande vizuri kabisa. Endapo utahifadhi kwa muda mrefu kwenye chocmbo cha kuokea mkate, funika na nailoni ya kufunikia chakula kwa juu

Enjoy

 

6 Replies to “Ice cream ya cookies na ndizi”

Leave a Reply