Dengu za nazi na curry

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 45
Muda jumla; dakika 55

Mahitaji

Kikombe 1 dengu kavu
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya kupikia
Kikombe 1 tui la nazi
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu 1 cha wastani
Kijiko 1 cha chakula nyanya ya kopo (au tomato sauce)
½ kijiko cha chai unga wa pilipili ya kukausha
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
½ kijiko cha chai mdalasini wa unga
Vijiko 2 vya chai curry powder
Kijiko 1 cha chakula vegetable au chicken bouillon powder/ cubes
¾ kijiko cha chai tangawizi
¾ kijiko cha chai kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula majani ya giligilani

Maelekezo

Osha na kuchuja dengu, weka pembeni

Katakata nyanya, kitunguu na majani ya giligilani; twanga kitunguu saumu na tangawizi,  weka pembeni

Weka nyanya na kitunguu kwenye mashine ya kusagia chakula utengeneze rojo. Endapo hutatumia mashine, utakapokatakata nyanya na vitunguu, kata vipande vidogovidogo sana

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, weka mafuta. Kaanga kitunguu saumu na tangawizi mpaka vilainike, kama dakika 3

Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu, nyanya ya kopo, curry powder, binzari ya pilau, unga wa giligilani, vegetable au chicken bouillon powder/ cubes na unga wa pilipili ya kukausha. Acha mchanganyiko upike kwa dakika kama 5, au mpaka nyanya ziive vizuri

Ongeza vikombe 2 vya maji na dengu kwenye sufuria, changanya vizuri

Funika sufuria, acha dengu ziive katika moto wa chini kwa dakika 20-30,

Au mpaka dengu ziive kabisa

Ongeza tui la nazi, acha tui liive kwa dakika 5 hadi 7 zaidi

Weka majani ya giligilani na kuipua

Pakua kama utakavyopenda

Leave a Reply