Kachumbari ya mtindi, tango na majani ya mnanaa

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Kikombe 1 mtindi mzito. Kutengeneza mtindi mzito bonyeza hapa
¼ kikombe majani ya mnanaa
½ ya tango
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
¼ kijiko cha chai sukari
Udaha (cayenne pepper) kiasi
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Kwangua tango kwenye kikwangulio na katakata majani ya mnanaa vipande vidogovidogo sana. Kama tango lina maji mengi, chuja maji

Changanya viungo vyote kwenye bakuli. Weka chumvi kwa kuonja

Pakua kama inavyohitajika

Enjoy na biryani ya nyama ya kusaga au biryani ya chicken tikka

Leave a Reply