Nanasi la kukaanga na mdalasini

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Nanasi 1, lililokatwakatwa vipande virefu
½ kikombe sukari ya brown
½ kikombe siagi
Kijiko 1 cha chai mdalasini

Maelekezo

Yeyusha siagi kwenye kibakuli kidogo. Changanya sukari na mdalasini kwenye siagi, weka pembeni

Kwenye kikaangio kizito katika moto wa juu kiasi, weka vipande vya nanasi. Nyunyizia mdalasini kiasi kwa juu

Paka mchanganyiko wa sukari na mdalasini juu ya mananasi

Kaanga/ choma nanasi kwa dakika kama 3 hadi 4 kwa kila upande, au mpaka pande zote zianze kupata rangi ya kahawia

Enjoy

 

Leave a Reply