Sambusa za manda za samli za bila kuchoma

Maandalizi; dakika 30
Muda wa kupika; dakika 40
Muda jumla; lisaa 1 dakika 10

Mahitaji

Manda za sambusa

Vikombe 1½ unga wa ngano
Vijiko 3 vya chakula samli
Kijiko 1 cha chai mbegu za jira/ cumin seeds
¼ kikombe pamoja na vijiko 3 vya chakula maji
Chumvi kwa kuonja

Mahitaji ya nyama

500g/ nusu kilo nyama ya kusaga
Hoho nusu x3 (kijani, njano na nyekundu)
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chakula tangawizi
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu
½ kikombe majani ya giligilani
½ kikombe majani ya kitunguu
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia (ukipenda)
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Mafuta ya kukaangia

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, chumvi, mbegu za jira na mafuta ya samli. Changanya vizuri kwa mkono mpaka uwe kama chenga chenga

Ongeza robo kikombe cha maji uanze kukanda, endelea kuongeza kijiko kimoja kimoja cha maji mpaka unga ushikane vizuri. Kanda hadi ulainike kabisa. Unga utakuwa mgumu kiasi ukilinganisha na wa chapati.

Funika bakuli na kitambaa kisafi cha jikoni, acha unga utulie kwa dakika kama 30

Wakati unga unatulia, anza kutengeneza nyama za kujaza sambusa. Katakata kitunguu na hoho vipande vya mraba vidogovidogo sana. Twanga kitunguu saumu na tangawizi; katakata majani ya giligilani na majani ya kitunguu vipande vidogovidogo sana. Weka pembeni

Kwenye kikaangio katika moto wa wastani, weka nyama, tangawizi na kitunguu saumu. Weka chumvi na pilipili manga kwenye nyama. Endapo nyama ni kavu ongeza vijiko 2 vya chakula vya mafuta; kama nyama ina mafuta usiweke mafuta

Pika mpaka nyama iive vizuri, huku ukigeuza geuza, kama dakika 15. Ikiiva ongeza kitunguu maji na hoho. Pika kwa dakika kama 2 nyingine

Ongeza majani ya kitunguu. Pika kwa dakika nyingine 1 huku ukigeuzageuza

Ipua, weka nyama kwenye bakuli. Changanya na majani ya giligilani, weka pembeni

Kanda unga tena, ugawanye kweye madonge ya mduara 6. Weka madonge ya unga kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga, acha yapumzike kwa dakika chache

Sukuma kila donge utengeneze umbo la mduara kama la chapati; nyembamba kuliko chapati

Kata katitaki upate vipande viwili vilivyolingana

Kunja upande mmoja wa unga hadi katikati

Paka maji kwa mkono au brush upande wa juu ulipokunja kwa mwanzoni, usipake mpaka mwisho

Kunja na upande mwingine ufunike upande uliokunja mwanzoni ambao umepakwa maji kwa juu. Tengeneza kama umbo la koni

Hakikisha umefunga vizuri hakuna tobo kwa chini

Jaza kijiko na nusu hadi vijiko viwili vya nyama. Usijaze sana, ukijaza sana itakuwa ngumu kufunga sambusa vizuri. Hakikisha unabakiza nafasi ya kufungia

Paka maji kona za sambusa kwa vidole au brush

Sukuma upande wa manda uliobebana kwa ndani kufunika nyama

Funga upande wa juu ambao una ubichiubichi wa maji. Hakikisha sambusa imefunga kabisa

Rudia na sambusa nyingine hadi umalize

Kwenye kikaangio katika moto wa wastani, chemsha mafuta ya kukaangia. Ongeza sambusa chache chache, hakikisha huzijazi sana zikasongamana

Inategemea na sambusa zinaliwa wakati gani; kama unaziandaa kwa ajili ya kuliwa baadae, zitoe kwenye mafuta zikianza kupata rangi ya kahawia

Hifadhi kwenye friji mpaka muda utakapozihitaji

Ukiwa tayari kuzitenga, zikaange katika moto wa wastani mpaka ziwe na rangi ya kahawia. Kama unatengeneza kuliwa hapohapo, kaanga mpaka ziwe za kahawia moja kwa moja

Hamishia kwenye sahani iliyowekewa tissues kwa juu ili kunyonya mafuta

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

 

19 Replies to “Sambusa za manda za samli za bila kuchoma”

Leave a Reply