Ice cream ya cookies na mint

Kutengeneza; dakika 15
Kugandisha; masaa 6
Muda jumla; Masaa 6 dakika 15

Mahitaji

Vikombe 2 whipping cream
Kikombe 1 maziwa ya sona (sweet condensed milk)
Cookies za chocolate 20
Kijiko 1 cha chai vanilla
Kijiko 1 hadi 2 cha chai radha ya mint au matonye (drops) 6 za peppermint oil
Kijiko 1 cha chai rangi ya kijani

Maelekezo

Weka cookies kwenye mfuko wa plastic wa kuhifadhia chakula. Acha hewa itoke, funga mfuko. Tumia kikaangio au kimti cha kusukumia chapati kuvunjavunja cookies, ila zisipodeke sana, ziwe na vipande vikubwa vikubwa, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, kwa kutumia mashine ya kusagia keki, piga cream, rangi ya kijani, radha ya mint na vanilla extract pamoja mpaka iwe nzito kabisa. (ongeza na kupunguza rangi na radha ya mint kutokana na upendeleo wako)

Ongeza maziwa ya sona, koroga vizuri kabisa

Weka cookies zilizovunjwavunjwa, koroga kiasi na kijiko

Mwagia mchanganyiko kwenye contena ya plastic yenye mfuniko au chombo cha kuokea mkate cha bati

Gandisha kwa masaa kadhaa au usiku kucha mpaka igande vizuri kabisa. Ikiwa tayari kuliwa, acha iyeyuke kwa dakika 5 hadi 10 iwe rahisi kuchota na kijiko

Enjoy

Leave a Reply