Kachumbari/ Chachandu ya mtindi na majani ya bizari

Maandalizi; dakika 5
Muda jumla; dakika 5

Mahitaji

¼ kikombe mtindi mzito, kuchuja mtindi recipe bonyeza hapa
Kijiko 1 cha chakula majani ya bizari (dill leaves)
Kijiko 1 cha chakula maji ya limao
¼ kijiko cha chai kitunguu saumu
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Katakata majani ya bizari (dill leaves); twanga kitunguu saumu

Kwenye kibakuli cha wastani, changanya viungo vyote ukoroge vizuri

Kula kama itakavyohitajika; ni nzuri sana kwa bhajiya za mbaazi

One Reply to “Kachumbari/ Chachandu ya mtindi na majani ya bizari”

Leave a Reply