Salad ya steki ya ndimu na pilipili hoho

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; Masaa 2 dakika 30

Mahitaji

Kwa marinade/dressing

500g/ nusu kilo steki ya nyama
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni
⅓ kikombe maji ya ndimu
Vijiko 2 vya chakula majani ya giligilani
Kijiko 1 kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai sukari ya brown
¾ kijiko cha chai pilipili ya kukausha
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
Kijiko 1 cha chai chumvi

Kwa salad

Nusu x 3 hoho rangi tofauti (nyekundu, njano, kijani)
Kitunguu maji 1 kikubwa
Vikombe 4 majani ya salad chaguo lako
Nyanya 1 ndogo
Parachichi 1
Majani ya giligilani ya kuweka juu
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kukaangia

Maelekezo

Tengeneza nusu ya kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako

Twanga kitunguu saumu, kamua ndimu na kukatakata majani ya giligilani

Kwenye bakuli ndogo, changanya vizuri viungo vyote vya marinade/ dressing

Weka nusu ya marinade/ dressing na nyama kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula kwenye jokofu au tumia bakuli kubwa, changanya vizuri. Funika bakuli/ funga mfuko, acha viungo vikolee kwa masaa 2 au vizuri zaidi usiku kucha. Toa nyama kwenye jokofu dakika 30 kabla ya kupika

Hifadhi marinade/ dressing iliyobakia kwenye jokofu kwa kutumia kwenye salad

Osha na kukausha majani ya salad; katakata nyanya, kitunguu, parachichi, hoho na majani ya giligilani

Kwenye kikaangio katika moto mkali kiasi, chemsha mafuta. Ongeza nyama kwenye mafuta

Acha nyama iive kila upande mpaka utakavyopenda wewe

Ipua nyama, acha ipoe

Wakati nyama inapoa, futa kikaangio. Ongeza kijiko cha chai cha mafuta, halafu kaanga hoho na nusu ya kitunguu kitunguu mpaka viive kama unavyopenda wewe

Katakata nyama vipande vyembamba

Pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda. Nyunyizia marinade/ dressing iliyobakia kwa juu na majani ya giligilani kwa juu

Enjoy

Leave a Reply