Biryani ya nyama ya mbuzi

Maandalizi; dakika 30
Muda wa kumarinate; masaa 4+
Muda wa kupika; lisaa 1 dakika 30
Muda jumla; Masaa 2

Mahitaji

Kwa wali

Vikombe 2 mchele wa basmati
½ kijiko cha chai mbegu za jira
Punje 4 za iliki
Bay leaf 1
Chumvi kwa kuonja

Kwa nyama

500g/ nusu kg nyama ya mbuzi
½ limao
Vijiko 1½ vya chakula majani ya kotimiri au giligilani
Vijiko 1½ vya chakula majani ya mnanaa
Vijiko 1½ vyaa chakula kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chakula tangawizi ya unga
¼ kikombe mafuta ya mzaituni
Chumvi kwa kuonja

Kwa kutengeneza sosi/ gravy

Nyanya 2 kubwa
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chai tangawizi ya unga
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu
Kipande cha mdalasini
Punje 4 karafuu
Punje 3 iliki
Bay leaf 1
½ kujiko cha chai mbegu za jira
½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha
Kijiko 1 cha chakula garam masala
Kijiko 1 cha chai unga wa giligilani
¾ kikombe mtindi
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya samli
Chumvi kwa kuonja

Viungo vya juu/ garnish

Kitunguu maji 1 cha wastani
Rangi ya zafarani kiasi
¼ kikombe maji ya uvuguvugu
Vijiko 2 vya chakula majani ya giligilani
Vijiko 2 vya chakula majani ya mnanaa
Vijiko 2 vya chakula majani ya bizari ukipenda (dill leaves)

Maelekezo

Hatua ya kwanza; Kumarinate nyama

Andaa viungo vya marinate; Katakata majani ya kotmiri au majani ya giligilani; kamua limao; twanga kitunguu saumu

Kwenye bakuli kubwa, changanya nyama na viungo vyote vya marinade vizuri

Funika bakuli uhifadhi kwenye jokofu, acha viungo vikolee kwa masaa kama manne au vizuri zaidi usiku kucha

Hatua ya pili; Maandalizi

Andaa mchele kwa kuuosha hadi maji yawe masafi kabisa. Loweka kwenye maji kwa muda wa dakika 30. Ukiloana, chuja maji weka pembeni

Andaa viungo vya sosi/ gravy; katakata nyanya na kitunguu vipande vidogovidogo vya mraba; twanga kitunguu saumu, weka pembeni

Andaa viungo kwa ajili ya juu/ garnish; Katakata kitunguu maji vipande virefu; katakata na majani ya giligilani, majani ya bizari na majani ya mnanaa

Loweka zafarani chache kwenye ¼ kikombe cha maji ya uvuguvugu. Weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa juu kiasi, chemsha vikombe 4 vya maji. Ongeza mchele, mbegu za jira, iliki, bay leaf na chumvi. Pika mpaka wali ukaribie kuiva.

Ipua, chuja maji. Weka pembeni

Hatua ya tatu; Kupika

Washa oven katika joto la 150 degrees C. Kwenye sufuria katika moto wa wastani kaanga kitunguu cha kuweka juu/ garnish mpaka kiwe na rangi ya kahawia ila kisiungue

Toa kitunguu kwenye mafuta, hamishia vitunguu kwenye sahani iliyotandazwa tissues za jikoni au chujio la bati ili mafuta yachuje. Weka pembeni kwa ajili ya kuweka juu ya biryani badae

Kwenye sufuria nyingine moto wa chini kiasi, weka mafuta ya samli. Yakichemka ongeza kitunguu saumu, pika mpaka kilainike dakika kama 2, halafu uongeze viuingo vizimavizima; karafuu, iliki, mdalasini, bay leaf na mbegu za jira. Kaanga kwa dakika kama 2 nyingine

Ongeza kitunguu maji, nyanya na viungo vikavu vilivyoandaliwa kwa ajili ya sosi; giligilani ya unga, tangawizi ya unga, pilipili ya kukausha na garam masala. Acha ipike mpaka nyama ziive vizuri

Ongeza nyama. Kaanga kwa dakika kama 10, huku ukigeuza geuza

Ongeza ¾ kikombe cha mtindi. Ongeza na chumvi kwa kuonja

Funika sufuria acha nyama iive taratibu kwa dakika 20 hadi 30, ukigeuza inapobidi. Ikiiva na kulainika vizuri, kutabakia sosi kiasi kwa ajili ya kuwivisha wali

Hatua ya 4; kupangilia biryani

Katika chombo cha kuokea sufuria nyingine kubwa zaidi sambaza nyama chini

Sambaza wali juu ya nyama

Ongeza na majani ya giligilani, majani ya bizari na majani ya mnanaa yaliyakatwakatwa kwa ajili ya kuweka juu pamoja na kitunguu cha kukaanga. Nyunyizia kwa juu maji yenye zafarani

Funika na foil

Acha wali uive kwenye oven iliyopata moto kwa dakika 20 hadi 30; au mpaka wali uive vizuri. (unaweza pia kupalilia kwa mkaa, au kuoka kwenye oven katika chombo chenye mfuniko)

Changanya vizuri

Tenga cha moto na kachumbari ya mtindi tango na majani ya mnanaa au ya tango na mtindi

Enjoy

 

4 Replies to “Biryani ya nyama ya mbuzi”

Leave a Reply