Pasta zenye sausage, brokoli na jibini

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Vikombe 2 vya pasta (fusilli)
250g/ robo kilo sausages
Vikombe 2 broccoli
Kikombe 1 hoho
Vikombe 2 maji
Vijiko 1½ vya chai beef bouillon powder/ beef flavor cube
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya kupikia
Kikombe 1 jibini (cheddar cheese)
Vijiko 2 vya chakula siagi
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Andaa viungo; katakata sausages, hoho na broccoli. Twanga kitunguu saumu, weka pembeni

Kwangua jibini, weka pembeni

Changanya maji na beef bouillon powder/ beef flavoured cube, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa juu, chemsha maji uweke na chumvi. Ongeza pasta uzichemshe kutokana na maelekezo ya kwenye pakiti. Chuja maji, weka pembeni

Kwenye sufuria kubwa au kikaango kikubwa katika moto wa juu kiasi, kaanga sausages na kitunguu saumu kwenye mafuta yaliyochemka. Pika kwa dakika kama 3 au mpaka harufu ya ubichi iishe kwenye kitunguu saumu na sausages zipate rangi ya kahawia kiasi

Ongeza mchanganyiko wa maji na beef bouillon powder. Acha ichemke katika moto wa juu kwa dakika kama 2 hadi 3

Ongeza broccoli na hoho. Funika acha ziive kwa dakika 3 hadi 4, au mpaka mboga ziive kama unavyopendelea

Ongeza siagi, jibini, chumvi na pilipili manga. Acha ichemke mpaka sosi iwe nzito

Changanya pasta zilizochemshwa, pakua haraka

Enjoy

 

4 Replies to “Pasta zenye sausage, brokoli na jibini”

    1. Sepermarkets au maduka ya vyakula. Kuna za maggi (powders na cubes), na nyingine tofauti. Unatumia moja kati ya hizo, beef bouillon powder ambayo ni unga au beef flavor cubes ambazi ni kama vidonge vya mraba

Leave a Reply