Supu ya minofu ya samaki na mbogamboga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

500g/ nusu kilo minofu ya samaki
Kijiko 1 cha chakula siagi
Kitunguu 1 cha wastani
½ kijiko cha chai kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chai chicken bouillon powder/ chicken flavored cubes
Vikombe 3½ maji
½ karoti
½ kikombe njegere
½ kikombe mahindi mabichi
¼ kikombe kitunguu cha majani ukipenda
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
½ kijiko cha chai dried basil
¼ kijiko cha chai dried oregano
Majani ya giligilni na limao ukipenda

Maelekezo

Andaa viungo; twanga kitunguu saumu; katakata kitunguu maji, karoti na majani ya kitunguu. Weka pembeni

Katakata samaki vipande vya kutosha kuingia mdomoni, weka pembeni

Changana vikombe 3½ vya maji na chicken bouillon powder/ chicken flavoured cubes, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, kaanga kitunguu saumu na kitunguu maji katika siagi iliyoyeyusha. Pika hadi kitunguu saumu kianze kuwa na rangi ya kahawia, dakika 2 hadi 3

Ongeza karoti, basil, oregano, mahindi, njegere na mchanganyiko wa maji na chicken bouillon powder. Pika hadi ichemke kabisa

Funika sufuria, acha iive moto wa chini kwa dakika 6 hadi 8

Ongeza samaki. Acha samaki aive bila kufunika kwa dakika 5 mpaka 7; au hadi samaki aive vizuri kabisa. Geuza mara chache inapobidi

Ongeza majani ya kitunguu. Weka chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Pakua na majani ya giligilani na vipande vya limao

Enjoy

4 Replies to “Supu ya minofu ya samaki na mbogamboga”

Leave a Reply