Kamba wa nazi

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

500g/ nusu kilo kamba
Nyanya 2
Kitunguu maji 1
¼ kikombe majani ya kotimiri au giligilani
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Kijiko 1 cha chai giligilani ya unga
½ kijiko cha chai binzari ya pilau
¼ kijiko cha chai pilipili ya unga (cayenne pepper)
Vikombe 1½ tui la nazi
½ kikombe maji
Ndimu 1
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Andaa viungo; twanga kitunguu saumu na tangawizi; katakata majani ya giligilani na kuosha Kamba

Weka kitunguu na nyanya kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, chemsha mafuta ukaange kitunguu saumu na tangawizi kwa dakika kama 2, au hadi vilainike vizuri

Ongeza rojo ya nyanya na kitunguu maji, giligilani ya unga, binzari ya pilau, pilipili ya unga na chumvi kwa kuonja

Funika sufuria acha nyanya ziive

Geuza mara chache mpaka ziive vizuri kabisa

Zikiiva, ongeza tui la nazi na maji. Acha ichemke moto wa chini kiasi kwa dakika 8 hadi 10, au mpaka sosi iwe nzito

Ongeza Kamba, pika kwa dakika kama 5 nyingine; au mpaka waive vizuri

Ongeza majani ya giligilani au kotimiri

Pakua ya moto na ndimu

Enjoy

One Reply to “Kamba wa nazi”

Leave a Reply