Salad rahisi ya kigiriki

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

½ kikombe pilipili hoho nyekundu
¼ kikombe mbegu za mzaituni za chaguo lako
Nyanya 1 ya wastani
½ kitunguu maji
Vijiko 1½ vya chakula majani ya kotimiri
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Kijiko 1 cha chakula siki (red wine vinegar)
½ kijiko cha chai dried oregano
¼ kikombe jibini (feta cheese)
½ tango
Chunvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Tengeneza kitunguu maji kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako

Andaa viungo; toa mbegu na kukatakata nyanya, tango na hoho vipande vidogovidogo vya mraba; katakata  jibini (feta cheese) vipande vidogovidogo vya mraba; katakata matunda ya mzaituni (olives) mara mbili kwa urefu na katakata na majani ya kotimiri

Changanya viungo vyote kwenye bakuli kubwa isipokuwa jibini. Hakikisha vimechanganyika vizuri

Ongeza chumvi na pilipili manga kwa kuonja. Ongeza jibini, changanya taratibu kwa uangalifu isibondeke

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

4 Replies to “Salad rahisi ya kigiriki”

Leave a Reply