Dressing ya salad ya ndimu na tangawizi

Maandalizi; dakika 10
Muda jumla; dakika 10

Mahitaji

Ndimu 1, maganda na maji yake
¼ kijiko cha chai tangawizi
Vijiko 2 vya chakula siki (red wine vinegar)
Kijiko 1 cha chai sosi ya soya
Vijiko vitatu vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Kijiko kimoja cha chakula asali
¼ kijiko cha chai chumvi
¼ kijiko cha chai pilipili ya kukausha

Maelekezo

Andaa viungo; kwangua ndimu; kamua maji ya ndimu; menya na kutwanga tangawizi

Changanya vizuri viungo vyote vizuri kwenye kibakuli kidogo au chupa ya kuchanganyia dressing

Tumia kama itakavyohitajika, kama kwenye salad ya mishikaki tandoori chicken; au salads nyingine tofauti

Enjoy

 

Leave a Reply