Salad ya mishikaki ya tandoori chicken

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Vikombe 4 majani ya salad chaguo lako
Nyanya ndogondogo kikombe 1
Kitunguu maji 1
Embe 1
¾ kikombe jibini (feta cheese)
Majani ya kotimiri ya kuweka juu
Mishikaki ya tandoori chicken; recipe bofya hapa
Dressing ya ndimu na tangawizi; recipe bofya hapa

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako

Oka au choma mishikaki ya tandoori chicken, bofya hapa kwa recipe

Tengeneza dressing ya ndimu na tangawizi, kwa recipe bonyeza hapa

Andaa viungo vingine; katakata embe na jibini vipande vidogovidogo vya mraba; katakata nyanya nusunusu; katakata majani ya kotimiri

Osha na kukausha majani ya salad

Pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda

Ongeza mishikaki ya tandoori chicken kwa juu, nyunyizia dressing ya ndimu na tangawizi. Mwagia na majani ya kotimiri kiasi kwa juu

Enjoy

 

Leave a Reply