Kachumbari ya tango, nyanya, kitunguu na mtindi

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Kikombe 1 tango
¾ kikombe mtindi mzito
½ kikombe nyanya
¼ kikombe kitunguu maji
Vijiko 2 vya chakula majani ya kotimiri
Vijiko 2 vya chakula majani ya mnanaa
½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha
Kijiko 1 hadi 2 vya chakula maji ya limao
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako. Chuja maji weka pembeni

Menya tango; toa mbegu na katakata tango na nyanya; katakata majani ya mnanaa na majani ya kotimiri

Saga majani ya mnanaa, majani ya kotimiri na maji ya limao kutengeneza rojo

Kwenye bakuli la wastani changanya viungo vyote. Ongeza chumvi kwa kuonja

Enjoy na biryani ya nyama ya kusaga, biryani ya chicken tikka, biryani ya mbuzi au biryani ya tandoori chicken

Enjoy

Leave a Reply