Egg chop kwenye sosi ya mtindi

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Kitunguu maji 1 kikubwa
Vijiko 2 vya chai kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chai tangawizi
Nyanya 3 za wastani
Kijiko 1 cha chai mdalasini wa unga
Kijiki 1 cha chai bizari ya pilau
½ kijiko cha chai bizari ya manjano
½ kijiko cha chai pilipili ya unga (cayenne pepper)
Kijiko 1 cha chai garam masala iliyosagwa
Vijiko 8 vya chakula maziwa ya mgando (mtindi)
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Chumvi kwa kuonja
Egg chops 6, kwa recipe ya egg chops bonyeza hapa
Majani ya kotimiri ya kuweka kwa juu

Maelekezo

Andaa viungo; katakata kitunguu maji na majani ya kotimiri. Twanga tangawizi na kitunguu saumu, weka pembeni

Weka nyanya kwenye mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, weka kitunguu ukikaange mpaka kiive, ila kisikauke. Ongeza tangawizi na kitunguu saumu. Kaanga mpaka harufu ya ubichi iishe na vilainike, kama dakika 2 nyingine

Ongeza rojo ya nyanya, garam masala, pilipili ya unga, mdalasini wa unga, binzari ya pilau and bizari ya manjano. Changanya vizuri halafu funika na mfuniko

Acha mchanganyiko uive katika moto wa chini huku zimefunikwa kwa dakika 6 hadi 8, au mpaka nyanya na viungo viive vizuri kabisa

Ongeza mtindi na ½ kikombe cha maji. Pika kwa moto wa wastani kwa dakika 2 nyingine; halafu uweke egg chops taratibu, uzigeuze zipate sosi pande zote. Kuwa muangalifu zisibomoke. Acha mchanganyiko uive kwa dakika moja nyingine

Nyunyizia majani ya kotimiri kwa juu, pakua kama utakavyopenda

Enjoy

Leave a Reply