Smoothie ya tikiti maji, strawberries na maji ya ndimu

Maandalizi; dakika 10
Muda jumla; dakika 10

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Vikombe 4 tikiti maji
Vikombe 4 strawberries zilizogandishwa
Vijiko 2 vya chakula maji ya ndimu
Majani 6 makubwa ya mint
Kijiko 1-2 vya chakula asali (ukipenda)

Maelekezo

Gandisha strawberries masaa 4 kabla ya kusaga; toa mbegu na kukatakata tikiti maji; kamua maji ya ndimu

Saga viungo vyote kwenye blender au mashine ya kusagia chakula hadi ilainike. (Endapo hutatumia strawberries zilizogandishwa, ongeza vikombe 3-4 vya barafu kwenye blender)

Tenga kama utakavyopenda

Enjoy

 

2 Replies to “Smoothie ya tikiti maji, strawberries na maji ya ndimu”

Leave a Reply