Chapati mchambuko za samli

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kusubiri; dakika 40
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; lisaa 1 dakika 10

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Vikombe 1½ unga wa ngano
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya samli ya kukandia
Vijiko 3 vya chai mafuta ya samli ya kukunjia, na ya ziada ya kukaangia
½ kikombe pamoja na vijiko 3 vya chakula maji
¾ kijiko cha chai chumvi

Maelekezo

Kwenye bakuli kubwa, changanya unga wa ngano, chumvi na vijiko 2 vya mafuta ya samli. Changanya vizuri kwa mkono mpaka uwe kama chenga chenga

Ongeza ½ kikombe cha maji uanze kukanda. Endelea kuongeza kijiko kimoja kimoja cha maji mpaka unga ulainike vizuri

Funika bakuli na kitambaa kisafi cha jikoni, acha unga utulie kwa dakika kama 15-30

Kanda unga tena, ugawanye kweye madonge 4 yaliyolingana

Weka madonge ya unga kwenye sehemu iliyonyunyiziwa unga, acha yapumzike kwa dakika chache

Sukuma kila donge hadi liwe jembamba kama chapati, au zaidi

Paka upande wa juu mafuta ya samli kiasi; kama ½ – ¾ kijiko cha chai

Kwa kutumia kisu kikali, kata kata unga vipande vyembamba sana kwa urefu. Ukikata vyembamba zaidi chapati inachambuka zaidi

Kusanya vipande vyote pamoja kwa ajili ya kukunja

Shikilia pande mbili za mwisho, vuta taratibu kufanya uwe mrefu zaidi kiasi uanze kukunja

Kunja hadi mwisho utengeneze umbo kama la koni. Dumbukiza ncha ya mwisho katikati kwa ndani  ili isifunguke. Rudia hadi umalize zote. Acha tena kwa dakika chache unga upumue

Nyunyizia unga usukume unga hadi zifikie ukubwa wa chapati

Kwenye kikaangio kilichochemka katika moto wa wastani, weka chapati. Acha ipike mpaka upande wa chini uwe na rangi ya kahawia kiasi na chapati ianze kutuna kiasi kwa juu

Geuza kwa upande mwingine. Paka mafuta ya samli juu ya chapati upande uliopikwa

Geuza tena upande mwingine, paka tena mafuta ya samli. Geuza tena pande zote mbili hadi chapati ziive vizuri, ziwe na rangi ya kahawia ila zisikauke

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

 

29 Replies to “Chapati mchambuko za samli”

  1. May God bless you dear, I’ve tried this at home and everyone was shocked since it was my first time to cook chapati but they were the yummiest ever and they wish I could coo them everyday, I used milk instead of water. Am soo thankful dear😚

    1. Thank you for a nice feedback, am very happy it worked out well. Next time I will go for milk too. Enjoy it with your family;)

Leave a Reply