Mishikaki ya kamba wa asali na nanasi

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

500g/ nusu kilo Kamba (shrimp au prawns)
Kikombe 1 nanasi fresh
Vijiko 3 vya chakula siagi
¼ kikombe asali
Kijiko 1 cha chakula kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula sosi ya soya
Kijiko 1 cha chakula maji ya limao
Chumvi na pilipili iliyopondwa (cracked pepper) kwa kuonja
Limao la kutenga na mishikaki
Vijiko 2 vya chakula majani ya kotimiri

Maelekezo

Kwenye sahani pana yenye shimo la kutosha au bakuli pana, loweka vijiti vya mishikaki kwa dakika kama 20 kabla ya kupika

Wakati vijiti vinalowana, andaa viungo vingine. Twanga kitunguu saumu; katakata nanasi vipande vya mraba ukubwa wa wastani; kamua maji limao; katakata majani ya kotimiri; katakata limao kwa ajili ya kutenga na mishikaki

Kwenye sufuria ndogo katika moto wa chini kiasi, yeyusha vijiko 2 vya siagi. Ongeza asali, sosi ya soya na kitunguu saumu mpaka ichanganyike vizuri. Acha ichemke moto wa chini kwa dakika 3-4, au mpaka sosi iwe nzito. Ipua kwenye jiko, ongeza maji ya limao

Panga Kamba na nanasi kwenye vijiki vya mishikaki kutengeneza mishikaki. Nyunyizia chumvi na pilipili iliyopondwa kwa kuonja,

Paka sosi ya asali na soya pande zote za mishikaki mpaka ikolee vizuri

Kwenye kikaangio katika moto wa wastani, yeyusha kijiko 1 cha siagi ilyobakia. Ongeza mishikaki. Pika mpaka ianze kubadilika rangi

Geuza upande wa pili, enyelea kupaka sosi huku inaendelea kuiva. Nyunyizia sosi ya kutosha

Pika kwa dakika 3 hadi 4, au mpaka Kamba waive vizuri na sosi ishike vizuri, kuwa muangalifu wasikae muda mrefu wakakauka

Pakua ya moto kama utakavyopenda na vipande vya limao. Nyunyizia na majani ya kotimiri kwa juu

Enjoy

Leave a Reply