Salad ya teriyaki chicken na nanasi la kukaanga

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 45

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Kwa kuku na salad

½ kikombe sosi ya teriyaki, bofya hapa kwa recipe
500g/ nusu kilo minofu ya kuku
Vikombe 4 majani ya salad chaguo lako
½ kikombe nyanya ndogondogo sana
Kitunguu maji 1 kidogo
Parachichi 1
Vipande kadhaa vya nanasi
Majani ya giligilani ya kuweka juu

Kwa dressing

½ kikombe sosi ya teriyaki, kwa recipe bofya hapa
⅓ kikombe siki (rice vinegar au apple cider vinegar)
⅓ mafuta ya mzaituni (olive oil)
¼ kikombe rojo ya nanasi la kusaga au juisi ya nanasi

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako.

Saga vipande vichache vya nanasi upate ½ kimombe rojo au juisi. Katika bakuli kubwa, changanya minofu ya kuku, ½ kikombe sosi ya teriyaki na ¼ kikombe rojo ya nanasi la kusaga au juisi ya nanasi. Changanya vizuri, acha viungo vikolee kwenye jokofu kwa dakika 15

Wakati kuku anakolea viungo. Kwenye bakuli ndogo au chupa ya dressing, changanya vizuri viungo vyote vya dressing. Hifadhi kwenye jokofu mpaka ikiwa tayari kutumiwa

Kwenye kikaangio kilichowekewa mafuta katika moto mkali kiasi, weka nyama ya kuku. Mwaga majimaji yatakayobakia hayahitajiki tena (vizuri ukitumia kikaangio kisichoshika chini)

Ongeza na vipande vya nanasi kwenye kikaangio. Pika nanasi hadi liwe la moto na kulainika.  Pika nyama ya kuku pande zote mbili mpaka iive vizuri

Hamishia nyama na nanasi kwenye kibao cha kukatia, acha ipoe kiasi

Wakati nyama na nanasi vinapoa, osha na kukausha majani ya salad; katakata nyanya nusunusu; katakata parachichi na majani ya giligilani

Katakata nyama vipande vyembamba. Pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda. Nyunyizia dressing kiasi utakachopenda kwa juu

Mwagia na majani ya giligilani kwa juu

Enjoy

 

Leave a Reply