Sosi ya teriyaki yenye nanasi, kitunguu saumu na tangawizi

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 5
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

¼ kikombe sosi ya soya
¼ kikombe maji
Kijiko 1 cha chakula corn flour/ cornstarch
Vijiko 4 vya chakula asali
Vijiko 3 vya chakula siki (apple cider vinegar)
Vijiko 4 vya chakula nanasi
Vijiko 2 vya chakula rojo ya nanasi la kusaga au juisi ya nanasi
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi

Maelekezo

Andaa viungo; twanga tangawizi na kitunguu saumu; tengeneza rojo ya nanasi la kusaga au juisi ya nanasi; katakata nanasi vipande vidogovidogo sana

Katika sufuria ndogo, changanya sosi ya soya, maji, corn flour/ corn starch, siki, kitunguu saumu, tangawizi, rojo ya nanasi la kusaga au juisi ya nanasi na vipande vya nanasi hadi ichanganyike vizuri

Chemsha mchanganyiko katika moto wa juu kiasi hadi upate moto. Ongeza asali kwenye sufuria mpaka ichanganyike vizuri

Punguza moto uwe wa wastani, endelea kuchemsha huku ukigeuzageuza mpaka upate uzito unaotaka

Tumia kama inavyohitajika. Kwa recipe ya salad ya teriyaki chicken bofya hapa

Enjoy

Leave a Reply