Pancakes rahisi za ndizi na oatmeal

Maandalizi; dakika 5
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 20

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Ndizi mbivu 2 za wastani
Mayai makubwa 2
½ kikombe oats
¼ kijiko cha chai mdalasini
¼ kijiko cha chai chumvi

Maelekezo

Weka oats kwenye blender au mashine ya kusagia chakula usage mpaka ziwe unga

Kwa kutumia uma au kijiko cha kupondea viazi, saga ndizi ndani ya bakuli mpaka zilainike

Ongeza mayai, oats zilizosagwa, mdalasini na chumvi uchanganye vizuri

Kwenye kikaangio katika moto wa chini, paka siagi kiasi. Ongeza ¼ kikombe cha mchanganyiko wa ndizi na oats kwenye kikaangio

Sambaza unga kiasi kutengeneza umbo la mduara kwa kutumia mgongo wa kijiko. Pika mpaka upande wa chini uwe wa kahawia kiasi na itune kiasi kwa juu

Tumia kijiko kipana kugeuza upande wa pili

Pika na upande mwingine mpaka uive vizuri

Pakua kama utakavyopenda na ndizi au matunda mengine; maple syrup au asali

Enjoy

Leave a Reply