Pizza ya tuna fish

 Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Mkate 1 wa pizza, jinsi ya kutengeneza bonyeza hapa
Kikombe 1-2 jibini (Mozzarella cheese)
¼ kikombe tomato sauce (ukipenda)
½ kikombe samaki wa kopo aina ya jodari (Tuna Fish) na mafuta yake
½ kitunguu cha wastani
¼ kikombe matunda ya mzaituni meusi (black olives)
Vipande 6-8 vya Salami (ukipenda)

Maelekezo

Washa oven yako moto wa 400°F au 200°C. Weka unga wa mkate kwenye sehemu iliyonyinyiziwa unga. Acha ukae kwa dakika chache. Jinsi ya kutengeneza unga wa mkate wa pizza bofya hapa

Sukuma unga wako hadi uwe mwembamba usawa wa chapati nyambamba (itakuwa pana kuliko chapati)

Weka kwenye chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta au karatasi za kuokea. Paka kona za mkate mafuta ya kwenye kopo la samaki

Paka tomato sauce kwa juu ya mkate mzima. (unaweza pia kupika bila tomato sauce)

Oka mkate na tomato sauce peke yake kwa dakika 8 hadi 10; halafu ongeza viungo vyote, pangilia kama utakavyopenda

Endapo utatumia salami, ongeza salami kwa juu na jibini nyingine ukipenda

Acha pizza iive kwa dakika 6 mpaka 10; au mpaka jibini iyeyuke na mkate uwe wa kahawia kiasi. Ipua na kukatakata kama utakavyopenda

Enjoy

 

 

4 Replies to “Pizza ya tuna fish”

Leave a Reply