Wali wa kukaanga wenye sausages na mbogamboga

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 25

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Vikombe 2 wali uliopikwa
Vikombe 1½ sausages
Kikombe 1 broccoli
½ kikombe pilipili hoho za rangi
½ kikombe uyoga (ukipenda)
½ kikombe vitunguu vya majani
Kitunguu maji 1 kidogo
Karoti 1
Vijiko 2 vya chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chakula mafuta ya ufuta
Vijiko 3 vya chakula sosi ya soya
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Mbegu za ufuta kiasi (ukipenda)

Maelekezo

Andaa viungo; katakata kitunguu, uyoga, karoti, hoho, brokoli, sausages na majani ya kitunguu; twanga kitunguu saumu, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa juu kiasi, chemsha mafuta kisha ukaange kitunguu kitunguu saumu hadi vilainike harufu ya ubichi iishe; kama dakika 2

Ongeza kitunguu maji na sausages. Kaanga mpaka kitunguu kiive na sausages zianze kupata rangi ya kahawia

Ongeza brokoli, karoti na hoho. Pika kwa dakika nyingine 3 hadi 4, ukigeuza mara kwa mara

Ongeza uyoga kama utatumia, pika kwa dakika 1 nyingine

Weka wali, soya sosi, vitunguu vya majani na mafuta ya ufuta. Pika kwa dakika kama 1 hadi 2 ukigeuza mara kwa mara

Pakua mara baada ya kuipua. Nyunyizia mbegu za ufuta kwa juu

Enjoy

6 Replies to “Wali wa kukaanga wenye sausages na mbogamboga”

  1. I have tried imetoka powa kweli although siku na soya sosi na hoho za rangi i only hade green ones. Thnx Jane

    1. Enjoy my dear, am happy imetokea vizuri. Unaweza tumia vegetables nyingine zozote unazopenda wewe, it works with everything;)

Leave a Reply