Bagia crispy za mbaazi (chickpea)

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kuloweka kunde; Usiku kucha
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30 + muda wa kuloweka

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Kikombe 1 mbaazi (chickpeas)
Kitunguu maji 1 kikubwa
Kikombe 1 chenga za mkate (bread crumbs)
¼ kikombe majani ya kotimiri
½ kijiko kitunguu saumu
Kijiko 1 tangawizi
Vijiko 3 vya chakula maji ya limao
Pilipili kichaa 2 (nyekundu na kijani ukipenda)
Kijiko 1 bizari ya pilau
Kijiko 1 cha chai baking soda
½ kijiko cha chai pilipili za kukausha
Chumvi kwa kuonja
Mafuta ya kukaangia

Maelekezo

Osha na kuloweka mbaazi angalau masaa 8, au usiku mzima ni nzuri zaidi. Ukiloweka zitaumuka zitakuwa kama vikombe viwili wakati wa kupika

Katakata kitunguu, pilipili na majani ya giligilani; twanga tangawizi na kitunguu saumu; kamua maji ya limao

Chuja mbaazi maji. Weka viungo vyote (isipokuwa mafuta na chenga za mkate) kwenye mashine ya kusagia chakula au blender hadi ilainike; Ila isilainike ikawa uji sana, bakiza chengachenga kiasi. (Unaweza pia kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu)

Hamishia mchanganyiko kwenye bakuli, ongeza chenga za mkate uchanganye vizuri

Funika bakuli, hifadhi kwenye jokofu kwa lisaa 1 hadi 2

Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani. Yakichemka, tumia vijiko 2 vya chakula kutengeneza umbo la mduara, au umbo utakalopenda wewe (unaweza tumia mkono pia)

Weka bagia kwenye mafuta

Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia

Toa bajia zilizoiva kwenye mafuta hamishia kwenye sahani iliyowekewa tissues, au chujio la bati ili mafuta yachuje

Pakua za moto kama utakavyopenda

Enjoy

6 Replies to “Bagia crispy za mbaazi (chickpea)”

    1. Inasaga bila tatizo, ila inategemea blender yako ina power kiasi, mimi natumia blender. Kama una wasiwasi tumia mashine ya mkono kama unayo

Leave a Reply to jane Cancel reply