Nyama ya kondoo ya kuoka na jibini na mbogamboga  

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya kwenye mstari kuona picha ya kiungo

Vipande vya nyama ya mbavu (lamb chops) kama 5
250g/ robo kilo jibini ya kupika (halloumi)
Kiazi kitamu 1 cha wastani
Vijiko 2 vya chakula majani ya rosemary
½ kikombe nyanya ndogondogo
Kitunguu maji 1 kikubwa
Mahindi mabichi 2 madogo
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
¼ mafuta ya kupikia
Zucchini ndogo 1
Pilipili mbuzi 1 (ukipenda)
¾ kijiko cha chai tangawizi ya unga
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai pilipili ya kukausha ukipenda
Majani ya kitunguu ukipenda

Maelekezo

Washa oven joto la 200°C (au andaa jiko la mkaa kwa ajili ya kuoka). Katakata viungo nyote vipande vikubwavikubwa; twanga kitunguu saumu; katakata majani ya rosemary na majani ya kitunguu vipande vyembamba

Weka viungo vyote katika bakuli kubwa (isipokuwa jibini na nyama). Changanya vizuri viungo vikolee kwenye mbogamboga

Paka nyama chumvi na pilipili manga

Katika chombo cha kuokea kilichopakwa mafuta, sambaza viungo vyote hakikisha havibebani sana

Oka kwa dakika 15 mpaka 20; au mpaka nyama iive kama utakavyopenda; mbohamboga ziive na jibini ipate rangi ya kahawia

Nyunyizia majani ya kitunguu kwa juu. Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

 

Leave a Reply