Rosti ya mbuzi na viungo mbalimbali

Recipe in english click here
Maandalizi; dakika 20
Muda wa kumarinate; usiku kucha
Muda wa kupika; dakika 40
Muda jumla; lisaa 1

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya viungo vyenye mstari kuona picha ya kiungo

Kwa nyama

500g/ nusu kg nyama ya mbuzi
½ limao
Vijiko 1½ vya chakula majani ya kotimiri au giligilani
Vijiko 1½ vya chakula majani ya mnanaa
Vijiko 1 vya chakula kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chakula tangawizi ya unga
¼ kikombe mafuta ya mzaituni (olive oil)
Chumvi kwa kuonja

Viungo vya rosti

Viazi ulaya vya wastani 3-4
Nyanya 2
Kitunguu 1 kikubwa
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula nyanya ya kopo
Pilipili kichaa 1
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya samli au mafuta ya kupikia
½ kikombe vitunguu vya majani
¾ kijiko cha chai tangawizi ya unga (au fresh)
Jani la bay 1 (bay leaf)
Karafuu punje 3
Iliki 3
Kijiko 1 cha chai giligilani ya unga (coriander powder)
Kipande cha mdalasini
Kijiko 1 cha chai garam masala
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Andaa viungo vya marinate; Katakata majani ya kotmiri au majani ya giligilani; kamua limao; twanga kitunguu saumu

Kwenye bakuli kubwa, changanya nyama na viungo vyote vya marinade vizuri. Funika bakuli, acha viungo vikolee kwa masaa kama manne au vizuri zaidi usiku kucha

Andaa viungo vya rosti; katakata viazi roborobo; kata pilipili vipande virefu; twanga kitunguu saumu; katakata majani ya kitunguu vipande vyembamba, weka pembeni

Weka nyanya na kitunguu katika mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo, weka pembeni

Kwenye sufuria katika moto wa wastani, weka mafuta ya samli. Yakichemka ongeza kitunguu saumu na viungo vizimavizima; karafuu, iliki na mdalasini. Kaanga kwa dakika kama 2; au mpaka kitunguu saumu kiive vizuri

Ongeza nyama iliyokuwa marinated. Kaanga kwa dakika kama 5, au mpaka iwe ya kahawia kiasi

Ongeza jani la bay (bay leaf) rojo ya nyanya pamoja na viungo vikavu; giligilani ya unga, tangawizi ya unga na garam masala. Ongeza na chumvi kwa kuonja. Pika mpaka nyanya ziive vizuri kabisa

Ongeza vikombe 2 maji. Funika na mfuniko, acha nyama iive moto wa chini kiasi kwa dakika 20 hadi 30; au mpaka ilainike kabisa na maji yaanze kukaukia

Ongeza viazi. Pika mpaka viazi viive vizuri na sosi iwe nzito

Ongeza majani ya kitunguu, pika kwa dakika 1 nyingine

Pakua kama utakavyopenda

Enjoy

11 Replies to “Rosti ya mbuzi na viungo mbalimbali”

Leave a Reply