Salad ya samaki, embe na chispi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 8
Muda jumla; dakika 38

Mahitaji

Kupata uhakika na kutumia viungo sahihi, endapo jina la kiungo limewekewa mstari, bofya viungo vyenye mstari kuona picha ya kiungo

Kwa salad

Vikombe 4 majani ya salad chaguo lako
Kikombe 1 nyanya ndogondogo
Kikombe 1 mahindi ya kopo (ukipenda)
Parachichi 1
Embe 1
Kitunguu maji 1 kidogo
Tortila chips kiasi chako
Majani ya kitunguu ya kuweka juu
Dressing ya ndimu na tangawizi, recipe bofya hapa

Kwa samaki

500g/ nusu kilo minofu ya samaki
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Vijiko 2 vya chakula maji ya ndimu
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya kupikia
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako

Andaa dressing ya ndimu na tangawizi kwa kubofya hapa, weka pembeni

Andaa viungo vya samaki, kamua maji ndimu; twanga kitunguu saumu na tangawizi, weka pembeni

Osha na kukausha samaki, mpake chumvi na pilipili manga, weka pembeni

Kwenye kibakuli kidogo, changanya kitunguu saumu, tangawizi, maji ya ndimu, pilipili manga na mafuta ya kupikia (olive oil)

Weka samaki kwenye sahani au bakuli pana, mwagia mchanganyiko wa kitunguu saumu na limao umpake vizuri. Funika, weka kwenye jokofu kwa dakika kama 15 viungo vikolee vizuri

Ukiwa tayari kupika, weka vijiko 2 vya mafuta mafuta kwenye kikaangio katika moto wa wastani. Vizuri kutumia kikaangio kisichoshika chini ili samaki asigande kwenye kikaangio

Pika samaki pande zote mbili mpaka aive vizuri

Hamishia samaki kwenye kibao cha kukatia, acha apoe kiasi halafu ukatekate

Wakati samaki anapoa, osha na kukausha majani ya salad

Katakata nyanya nusunusu; katakata parachichi, embe na majani ya kitunguu

Pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda

Nyunyizia dressing iliyobakia kwa juu. Mwagia majani ya kitunguu kwa juu

Tenga kama utakavyopenda

 

4 Replies to “Salad ya samaki, embe na chispi”

Leave a Reply