Boga la kuponda lenye mdalasini

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 20
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Vikombe 3 boga
Vijiko 2 hadi 3 vya chakula whipping cream au maziwa
Kijiko 1 cha chakula siagi
¼ kijiko cha chai mdalasini wa unga
Maple syrup kwa kuonja (au asali)
Chumvi kwa kuonja

Maelekezo

Menya, toa mbegu na kukatakata boga

Chemsha maji hadi yachemke vizuri. Ongeza boga, chemsha mpaka lilainike, dakika 10 hadi 12

Chuja maji boga

Weka boga kwenye bakuli. Ponda kwa kutumia kijiko cha kupotena viazi au saga kwa kutumia mashine ya mkono mpaka lilainike vizuri

Rudisha mchanganyiko kwenye sufuria. Ongeza whipping cream au maziwa kidogokidogo mpaka upate uzito utakaopenda. Ongeza maple syrup kwa kuonja na mdalasini

Changanya vizuri. Ongeza chumvi kwa kuonja

Enjoy

Leave a Reply