Salad ya kuku, parachichi na mozzarella cheese

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 15
Muda jumla; dakika 30

Mahitaji

Marinade/Dressing

¼ kikombe siki (balsamic vinegar)
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Vijiko 2 vya chai sukari ya brown
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai dried basil
Kijiko 1 cha chai chumvi

Kwa Salad

500g/ nusu kilo minofu ya kuku
Vikombe 4 majani ya salad chaguo lako
Parachichi 1
½ kikombe nyanya ndogondogo sana
Kitunguu maji 1 kidogo
½ kikombe jibini (mozzarella cheese)
Vitunguu vya majani kiasi
Chumvi na pilipili manga wa kuonja

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na jibini; chaguo lako

Kwenye bakuli ndogo au chupa ya dressing, changanya vizuri viungo vyote vya dressing

Kwenye bakuli kubwa, weka kuku. Mpake vijiko 4 vya mchanganyiko wa marinade/ dressing hadi akolee vizuri. Hifadhi dressing/ marinade itakayobakia kwa ajili ya salad badae

Kwenye kikaangio katika moto mkali kiasi, chemsha mafuta kisha weka nyama ya kuku. (vizuri ukitumia kikaangio kisichoshika chini). Pika kuku pande zote mbili mpaka iive vizuri

Hamishia nyama kwenye kibao cha kukatia, acha ipoe kiasi

Wakati nyama inapoa, osha na kukausha majani ya salad;

Katakata nyanya nusunusu; katakata parachichi, jibini na majani ya giligilani

Katakata nyama vipande vyembamba. Pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda

Nyunyizia dressing iliyobakia kwa juu. Mwagia majani ya kitunguu kwa juu

Enjoy

Leave a Reply