Tambi za nyama ya kusaga yenye mozzarella cheese

Maandalizi; dakika 30
Muda wa kupika; dakika 30
Muda jumla; lisaa 1

Mahitaji

Nyama na jibini (mozarella cheese)

500g/ nusu kilo nyama ya kusaga
Slesi 1 ya mkate
Yai 1
Kijiko 1 chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Pilipili kichaa 1
Kitunguu 1 cha wastani
250g/ robo kilo jibini (mozzarella cheese)
¼ kikome majani ya giligilani
Kijiko 1 cha chakula beef bouillon powder
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Vijiko 2 mafuta ya mzaituni (olive oil)

Tambi na sosi

250g/ nusu paketi ya tambi
Nyanya 1 kubwa
Kitunguu 1 cha wastani
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Kikombe 1 nyanya ya box (nyepesi)
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Kikombe 1 maji
½ kikombe mozzarella cheese
Majani ya giligilani kiasi
Jibini ya kunyinyizia kwa juu

Maelekezo

Weka nyanya na kitunguu kwenye mashine ya kusagia kutengeneza rojo; twanga kitunguu saumu na tangawizi kwa ajili ya sosi, weka pembeni

Katakata jibini (mozzarella cheese) vipande vidogovidogo vya mraba; twanga kitunguu saumu na tangawizi; katakata pilipili kichaa na majani ya giligilani vipande vidogovidogo sana; toa sehemu za pembeni kavu za mkate, katakata kipande cha katikati vipande vidogovidogo sana

Kwenye bakuli kubwa, weka nyama, mkate, kitunguu saumu, tangawizi, pilipili, majani ya giligilani, yai, kitunguu maji, beef bouillon powder, chumvi na pilipili manga, changanya vizuri kwa mkono

Gawanga nyama kwenye madonge madogomadogo kama 20

Weka kipande cha jibini katikati ya nyama, hakikisha kimefunikwa vizuri na nyama. Sawazisha vizuri kwa juu, weka pembeni

Kwenye sufuria au kikaangio kikubwa katika moto wa juu kiasi, chemsha vijiko 2 mafuta. Ongeza madonge ya nyama. Kaanga kwa dakika 1 hadi 2, au mpaka iwe ya kahawia kwa nje ila isiive kabisa

Hamisha nyama kwenye sahani

Chemsha tambi kutokana na maelekezo ya kwenye paketi, chuja maji, weka pembeni

Kwenye sufuria/ kikaangio ulichotumia kupika nyama, rudisha kwenye moto. Ongeza vijiko 2 vya chakula mafuta, yakichemka ongeza kitunguu saumu na tangawizi pika mpaka vilainike. Ongeza rojo ya nyanya na nyanya ya box, koroga vizuri. Funika na mfuniko, geuza ikibidi

Pika mpaka nyanya ziive vizuri

Ongeza kikombe 1 cha maji, acha yachemke mpaka sosi ianze kutokota. Ongeza nyama, pika kwa dakika 4 mpaka 5, au mpaka iive vzuri. Kuwa muangalifu isiive sana jibini ikaanza kuchuruzika kwa nje

Ongeza tambi zilizochemka, pika kwa dakika nyingine moja hadi 2. Weka majani ya giligilani. Toa kwenye moto, ongeza jibini kwa juu wakati bado ya moto sana

Pakua chakula kiliwe cha moto

Enjoy

 

 

2 Replies to “Tambi za nyama ya kusaga yenye mozzarella cheese”

Leave a Reply