Salad ya tuna fish na jibini

Maandalizi; dakika 15
Muda jumla; dakika 15

Mahitaji

Vikombe 4 majani ya salad
½ kikombe parmigiano reggiano cheese/ parmesan cheese (au jibini yoyote)
Kikombe 1 tuna fish ya kopo
Kikombe 1 nyanya ndogondogo
½ kikombe matunda ya mzaituni (olives)
Kitunguu maji 1 kidogo
Vijiko 2-3 vya chakula siki (balsamico vinegar)
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja

Maelekezo

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, kuloweka na limao au kuloweka na siki; chaguo lako

Katakata nyanya nusu nusu; katakata na salad vipande vidogovidogo

Pangilia viungo vyote kwenye bakuli la kutengea chakula mezani kama utakavyopenda

Nyunyizia chumvi na pilipili manga. Mwagia siki (baslamico vinegar) kwa juu

Enjoy

 

Leave a Reply