Mishikaki ya teriyaki chicken

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kumarinate; dakika 30 au usiku kucha
Muda wa kuchoma; dakika 10
Muda jumla; dakika 25 + muda wa kumarinate

Mahitaji

Marinade ya nyama

500g/ nusu kilo minofu ya kuku
¼ kikombe sukari ya brown
¼ kikombe soya sosi
Vijiko 3 vya chakula juisi ya nanasi
Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
Kijiko 1 cha chai tangawizi
Pilipili manga kwa kuonja
¼ kijiko cha chai chumvi
½ kijiko cha chai pilipili ya kukausha
½ kijiko cha chakula cornflour/ cornstarch
Vijiko 2 vya chakula maji

Kwa mishikaki

Nusu mara 3 hoho za rangirangi (kijani, njano, nyekundu)
Kitunguu maji 1 cha wastani
Vikombe 2 vipande vya nanasi
Majani ya kitunguu

Maelekezo

Osha, katakata na kukausha nyama ya kuku; twanga kitunguu saumu na tangawizi

Kwenye sufuria ndogo, changanya sukari, soya sosi, juisi ya nanasi, kitunguu saumu, tangawizi, pilipili manga, pilipili ya kukausha na chumvi. chemsha huku ukikoroga moto wa wastani mpaka sukari iyeyuke

Kwenye kibakuli kidogo, koroga vijiko 2 vya maji na cornflour/ cornstarch

Ongeza mchanganyiko wa cornflour/ cornstarch kwenye sufuria. Acha mchanganyiko kuchemke kwa dakika 1 hadi 2; au mpaka uanze kuwa mzito. Ipua, weka pembeni ipoe

Acha sosi ipoe, weka ¼ kikombe pembeni kwa ajili ya badae. Changanya nyama ya kuku na sosi iliyobakia vizuri kwenye bakuli au mfuko wa kuhifadhia chakula. Funika/ funga vizuri, weka kwenye jokofu viungo vikolee kwa dakika 30 mpaka usiku kucha

Ukiwa tayari kuoka. Katakata hoho, kutunguu na nanasi vipande vya mraba. Ongeza mafuta ya mzaituni/ olive oil changanya vizuri. Chomeka kuku na mchanganyiko wa nanasi na hoho kwenye vijiti vya mishikaki huku ukichanganyachanganya

Choma kwa dakika 8 hadi 10; au mpaka kuku aive. Kwa oven, oka kuku kwa dakika 30, dakika 15 kila upande. Paka sosi iliyobakia kwa juu wakati unageuza mishikaki ishike vizuri

Nyunyizia majani ya kitunguu kwa juu. Enjoy

 

Leave a Reply