Supu ya boga, karoti na cream

Maandalizi; dakika 10
Muda wa kupika; dakika 25
Muda jumla; Dakika 35

Mahitaji

Vikombe 2½ boga
Karoti 2 za wastani
Kijiko 1 mafuta ya kupikia
Kitunguu kimoja cha wastani
Kijiko 1½ cha chai chicken bouillon powder
Vikombe 2 vya maji ya moto
¼ kikombe whipped cream
Chumvi na pilipili manga kwa kuonja
Majani ya giligilani ya kuweka juu
Vijiko 2 vya chai whipping cream ya kutengea

Maelekezo kwa video

Maelekezo kwa picha

Katakata boga, karoti, kitunguu maji na majani ya giligilani

Kwenye sufuria katika moto wa wastani chemsha mafuta. Yakichemka ongeza kitunguu maji mpaka kiive ila kisikauke, kama dakika 1. Ongeza boga na karoti, kaanga kwa dakika kama 5

Punguza moto wa jiko, mimina maji na chicken bouillon powder kwenye sufuria. Funika sufuria

Acha ichemke kwa moto wa chini kwa dakika kama 12, au mpaka mboga zilainike, ipua

Kwa kutumia kijiko cha kubondea viazi au mashine ya mkono, au blender, saga mchanganyiko hadi uwe rojo

Rudisha mchanganyiko kwenye moto katika moto wa wastani. Ongeza wipping cream, chumvi na pilipili manga kwa kuonja. Endapo itakuwa nzito sana, ongeza maji au whipping cream kupata uzito utakaopenda

Pakua, weka majani ya giligilani na whipping cream kwa juu

Enjoy

2 Replies to “Supu ya boga, karoti na cream”

Leave a Reply