Mkate wa ndizi

Maandalizi; dakika 15
Muda wa kupika; dakika 35-50
Muda jumla; Dakika 50 mpaka lisaa 1 na dakika 5

Mahitaji

¾ kikombe sukari
½ kikombe siagi
Mayai 2
Kikombe 1 ndizi za kuponda (kama ndizi 2 za wastani)
1/3 kikombe maziwa
Kijiko 1 cha chai vanilla
Vikombe 2 unga wa ngano
Kijiko 1 cha chai baking soda
½ kijiko cha chai chumvi

Maelekezo

Washa oven joto la 175 degrees C. Paka siagi na unga wa ngano chombo cha kuokea mkate, weka pembeni

Kwenye bakuli jingine, tumia uma au kijiko cha kupondea viazi kuponda ndizi hadi zilainike, weka pembeni

Kwenye bakuli jingine pembeni, changanya au chekecha pamoja unga wa ngano, baking soda na chumvi, weka pembeni

Kwenye bakuli kubwa, changanya sukari na siagi hadi ilainike

Ongeza mayai, koroga vizuri

Ongeza vanilla

Ongeza maziwa, koroga vizuri hadi ichanganyike vizuri kabisa

Weka mchanganyiko wa unga wa ngano. Koroga hadi ilainike vizuri

Ongeza ndizi za kuponda,  koroga kwa kijiko zichanganyike vizuri

Mimina kwenye chombo cha kuokea

Oka kwa dakika 35 hadi 50 kutegemea na oven yako; au mpaka ukichomeka kijiti cha meno kinatoka kisafi. Acha ipoe kwenye chombo cha kuokea kwa dakika 5

Toa kwenye chombo cha kuokea.  Acha upoe kabisa kama kwa saa moja. Katakata na tanga kama utakavyopenda

Hifadhi kwenye friji ikiwa imefunikwa vizuri. Enjoy

16 Replies to “Mkate wa ndizi”

  1. Mimi naomba kujuwa unavyosema vikombe2 vya unga ni sawa na nusu au robo pia ukisema kikombe cha skri pia ni robo au vipo hivi vinanichanganya da jane

    1. Ukiweka mayai haikatiki, inaonekana imekatika kiasi sana ukiweka maziwa, ila ukishaweka unga inakuwa kawaida. Ilionekana imekatika mpaka mwishoni?

Leave a Reply