Salad ya kuku yenye asali na haradali

Maandalizi; dakika 15
Muda wa Marinate; masaa 2
Muda wa kupika; dakika 10
Muda jumla; Masaa 2 dakika 25

Mahitaji

Dressing / Marinade

⅓ kikombe asali
Vijiko 2 vya chakula mbegu za haradali
Vijiko 2 vya chakula sosi ya haradali (mild Dijon mustard)
Vijiko 2 vya chakula mafuta ya mzaituni (olive oil)
Kijiko kimoja cha chai kitunguu saumu
Chumvi kwa kuonja
400g minofu ya nyama ya kuku

Kwa salad (Tumia viungo utakavyopenda)

Majani ya salad
Nyanya ndogondogo
Parachichi moja kubwa
Ndimu ya kuosha kitunguu
Kitunguu maji 1 kidogo
Radish (Ukipenda)
Majani ya vitunguu (ukipenda)

Maelekezo

Menya na kutwanga kitunguu saumu

Weka viungo vyote vya marinade/ dressing kwenye bakuli la ukubwa wa wastani, isipokuwa kuku. Koroga hadi vichanganyike vizuri

Kwenye bakuli jingine weka minofu ya kuku. Mwagia nusu ya mchanganyiko wa marinade/dressing. Hakikisha Kuku anakolea viungo vizuri. Funika na hifadhi kwenye jokofu mchanganyiko wa marinade uliobaki, utumie badae kwenye salad

Funika bakuli vizuri, acha viungo vikolee kwa masaa mawili kwenye jokofu

Tengeneza kitunguu kwa kuosha na chumvi, ndimu/limao au siki

Kwenye kikaangio kisichoshika chini katika moto wa wastani, chemsha kijiko cha chakula mafuta ya kupikia. Ongeza minofu ya kuku

Pika kila upande hadi uwe na rangi ya kahawia na iive vizuri

Hamishia kuku kwenye kibao cha kukatia, acha ipoe kwa dakika chache

Wakati kuku anapoa, andaa viungo vya salad. Osha , katakata na kukausha majani ya salad; katakata nyanya, radish na parachichi. Katakata na majani ya vitunguu, weka pembeni

Ongeza vijiko viwili vya maji kwenye mchanganyiko wa marinade / dressing uliohifadhi kwenye jokofu

Katakata kuku katika vipande vipande, weka pembeni. Weka viungo vyote vya salad kwenye bakuli ya kutengea mezani kama utakavyopenda. Ongeza vipande vya kuku kwa juu

Nyunyizia dressing juu ya salad (kuwa muangalifu usizidishe, weka kiasi kwanza uongeze badae). Mwagia majani ya kitunguu; nyunyizia na chumvi na pilipili manga kwa juu ukipenda

Enjoy

 

 

 

Leave a Reply